NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.20 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2286.8 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.7.
Aidha, Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.3 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.84 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.07.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 23, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati huo huo, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2594.62 na kuuzwa kwa shilingi 2621.5.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3099.09 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3131.0022.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.655.
Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.02 na kuuzwa kwa shilingi 152.5 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.13 na kuuzwa kwa shilingi 20.29.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania