NA GODFREY NNKO
PAUNDI ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3062.05 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3093.6 na Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Aidha,dola ya Marekani nchini inanunuliwa kwa Shilingi 2286.823 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.7.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 25, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati huo huo, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2553.92 na kuuzwa kwa shilingi 2579.92 na Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.51 huku ikiuzwa kwa shilingi 365.05 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.12.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.24 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.04 na kuuzwa kwa shilingi 150.49 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.10 na kuuzwa kwa shilingi 20.27.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania