"Wawekezaji wote mnaowajibu wa kuhakikisha kuwa shughuli zenu za uchimbaji, uchenjuaji na uchakataji wa madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheris na taratibu ili tuweze kunufaika na madini yetu sambamba na nyinyi kupata faida,"Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ameyasema hayo Februari 22, 2022 wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.