WIZARA YA ARDHI YATOA SIKU 60 WENYE VIWANJA VILIVYOPIMWA KUWASILISHA MAOMBI YA KUMILIKISHWA

NA MUNIR SHEMWETA- WANMM

WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa siku 60 kuanzia tarehe 5 Februari, 2022 kuhakikisha wamiliki wa ardhi waliopimiwa viwanja wanawasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi huku wale wenye miliki za ardhi wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi ameyaeleza hayo leo Februari 4,2022 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Amesema, mmiliki ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa, Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kufuta miliki, kupiga mnada na kumilikisha viwanja vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.

‘’Mmiliki ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kufuta miliki, kupiga mnada na kumilikisha viwanja kwa wananchi wenye uhitaji, hatua hizi zitaanza kuchukuliwa Aprili 6,2022,"amesema Dkt.Kijazi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ni wajibu wa kisheria kwa wamiliki ambao ardhi zao zimepangwa na kupimwa kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi kwa Kamishna wa Ardhi ili kumilikishwa sambamba na kulipa kodi ya pango la ardjhi.

‘’Ni wajibu wa kisheria kwa wale wamiliki wa ardhi ambao ardhi zao zimepangwa na kupimwa kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi kwa Kamishna wa Ardhi kwa ajili ya kumilikishwa na kulipa kodi ya pango la ardhi,"amesema Dkt.Kijazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Wasilianeni na wadau wa ardhi kutafuta suluhisho la kwanini watu hawajimilikishi viwanja vilivyopimwa na hawalipi Kodi
    Mtanishukuru baadae
    Kufokea wadau ni utaratibu wa kisheria kabisa lakini haiwezi leta tija Kwa sababu za umangimeza wa watumishi wa ardhi

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news