NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro amesema
kuwa, wamedhamiria kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
kwa namna nyingine.
"Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ni kiongozi na mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi,kwa kutambua na kuenzi mchango wake Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa mpango mahususi wa kitaifa wa miaka 10 wa kuenzi na kutangaza urithi aliotuachia,"amesema Dkt.Ndumbaro.