52 wafukuzwa kazi kwa kughushi vyeti, kusema uongo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza limeridhia kufukuzwa kazi kwa watumishi 52 ambao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga amesema leo Machi 18, 2022 kuwa watumishi hao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kitumishi ikiwemo kusema uongo na kughushi vyeti.

Makaga amezitaka idara za elimu ya msingi na sekondari kujitathimini juu ya utendaji kazi huku akionya tabia ya wakuu wa idara hizo kuwahamisha wakuu wa shule na walimu wakuu wanaodaiwa kufanya ubadhirifu kwenye maeneo.

Makaga ametoa agizo kwa ofisa elimu Sekondari na msingi wa halmashauri hiyo kuwashusha vyeo walimu wakuu waliobainika kufanya ubadhirifu wa mali za umma katika vituo vyao vya kazi.

Diwani wa Kata ya Kasenyi, Triphone Marley amesema hakuna sababu ya watumishi wanaofanya makosa kwenye maeneo yao kuhamishwa vituo vya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Binuru Shekidele amesema atasimamia nidhamu ya watumishi Ili kulinda hadhi yao kukemea maovu yanayofanywa na baadhi ya watu wa halmashauri hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news