BETWAY yaendelea kukarabati viwanja vya mpira wa kikapu Dar

*TBF wapongeza hatua hiyo

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI inayoongoza Kimataifa katika kubashiri michezo mtandaoni, Betway ambayo ni sehemu ya Super Group, imekarabati na kuzindua kiwanja kingine cha mpira wa kikapu kilichopo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 26,2022 ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo kuboresha ya vituo vya michezo unaolenga kukarabati viwanja 5 vya mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam.

Kupitia mradi huo, Betway inakarabati viwanja vya mpira wa kikapu katika vituo vya michezo vya umma kwa nia ya kuongeza thamani ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini.

Ili kuhakikisha viwanja vilivyokarabatiwa vinatunzwa ipasavyo kwa matumizi endelevu, Betway inashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)–chombo cha serikali chenye jukumu la usimamizi wa mpira wa kikapu nchini.

TBF ina jukumu kubwa katika kuhakikisha kuwa viwanja hivi vinatumika ipasavyo kwa mashindano ya mpira wa vikapu na shughuli zingine zinazohusiana na mchezo huo.

Hafla hiyo ya uzinduzi imeenda sambamba na bonanza lililowaleta pamoja zaidi ya watu 250 na wadau kutoka sekta ya mchezo wa mpira wa kikapu wakijumuika kushuhudia uzinduzi wa kiwanja hicho.
Tukio kuu la bonanza hilo lilikuwa ni mchezo wa mpira wa kikapu kati ya timu 2 za kike, Dar Queens na Dar Divas wakiwania kitita cha THS 500,000. Betway iliwapa kipaumbele wanawake kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.

Akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi, Afisa Masoko wa Betway Tanzania, Calvin Mhina, alieleza kwa ufupi lengo la Betway kufanya maboresho ya viwanja.

"Tulichukua jukumu la kuongeza hadhi ya uwanja huu (Leaders Club) kwa kuzingatia thamani itakayoongeza kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwani huu ni moja ya viwanja maarufu vya michezo na burudani jijini Dar es Salaam. Betway tunaamini kuwa maendeleo ya jamii ni sehemu ya majukumu yetu ya msingi na tutaendelea kusaidia jamii ya wanamichezo katika nyanja zote za maendeleo ya michezo,”amesema Mhina.

Katibu Mkuu wa TBF, Mwenze Kabinda amepongeza hatua ya Betway huku akikiri kuwa kuboreshwa kwa uwanja huo kutaongeza thamani kubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu.

“Tukiwa kama shirikisho linalohusika na maendeleo ya mchezo huu, ni furaha kubwa kwetu kuona wadau kama Betway wanawekeza katika kuboresha miundombinu ambayo ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo ya mchezo wowote ule. Tunashukuru kwa mradi huu na hii inaleta msukumo kwetu kama mamlaka husika kuja na mashindano zaidi ili kuhakikisha viwanja hivi vinatumika,"amesema Mwenze.

Wachezaji wa mpira wa kikapu, wapenzi na wadau walioshiriki katika bonanza hilo walifurahi sana kutazama mchezo huo na kushiriki katika matukio mengine ya kuburudisha. Wachezaji pia walielezea furaha yao juu marekebisho ya uwanja waliyoyaona na kuwa sehemu ya uzinduzi kwa kucheza.

Kuhusu Betway Group

Betway ni sehemu ya Super Group: Kampuni ya kimataifa ya kidijitali ambayo hutoa burudani ya daraja la kwanza katika ulimwengu wa kubashiri na bahati nasibu.

Super Group (SGHC) Limited ni kampuni inayoongoza duniani katika biashara ya kubashiri michezo mtandaoni na bahati na nasibu: Betway, chapa kubwa ya kubashiri michezo mtandaoni na Kasino. 

Imeorodheshwa kwenye New York Stock Exchange (NYSE ticker: SGHC), kampunii imepewa leseni katika maeneo zaidi ya 20, ikiwa na nafasi za juu katika masoko makubwa kote Ulaya, Amerika na Afrika.

Mafanikio ya kikundi katika kubashiri michezo na bahati nasibu za mtandaoni yanachagizwa na teknolojia nzuri ili kuiwezesha kuingia haraka na kwa ufanisi katika masoko mapya.

Teknolojia yetu husaidia katika upembuzi yakinifu wa taarifa za masoko huiwezesha kutoa huduma za kipekee kwa wateja. Kwa maelezo zaidi, tembelea www.sghc.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news