NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah amesema fedha za kutekeleza miradi zilizoletwa mkoani hapa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022 ziwe chachu ya maendeleo kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Killimbah
aliyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa
Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika makao makuu ya chama hicho mkoani
hapa jana.
“Fedha
hizi zilizotetwa na Mama yetu katika mkoa wetu ziwe chachu ya maendeleo
kwa mwaka huu unaokuja,” alisema Killimbah huku akishangiliwa na mamia
ya wananchi na wana CCM waliohudhuria hafla hiyo.
Alisema,
miradi inayokuja mahala popote fedha hizo zinatafutwa na Rais wetu kwa
juhudi kubwa na wabunge wanasimamia bajeti ili ije Singida kwa ajili
ya kuleta maendeleo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, akihutubia kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika makao makuu ya chama hicho mkoani hapa jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniphace akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akizungumza kwenye hafla hiyo wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Hafla ikiendelea.
Killimbah
alitumia mkutano huo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo
makubwa ya maendeleo aliyoufanyia Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akizungumza kwenye hafla hiyo
alisema kwa mwaka mmoja alioongoza Rais Samia Suluhu Hassan Mkoa wa
Singida umepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwani wilaya zote wamepokea
fedha nyingi za maendeleo.
Alisema
sambamba na hilo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akikutana na makundi
mbalimbali kwa lengo la kuwasikiliza na kupokea maoni yao kwa ajili ya
kujenga nchi yetu na kuwa huo ni ukomavu mkubwa wa kisiasa na
kujiamini katika utendaji wake wa kuongoza nchi.
Hafla ikiendelea.
Viongozi wa CCM na Wazee wakiwa kwenye hafla hiyo.
Makofi yakipigwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniphace, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wakuu wa Idara za Serikali na Wataalamu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wakuu wa Idara za Serikali na Wataalamu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Vaileth Soka akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati
akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo alimfananisha Rais Samia
Suluhu Hassan na mwanamke mmoja shujaa aliyetajwa kwenye Biblia aitwaye
Esther ambaye alijulikana sana kwenye Taifa la Waisrael.
“Rais wetu Mama Samia amefanya mambo mema na makubwa katika nchi hii hivyo tunakila sababu ya kumpongeza” alisema Digha.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita alisema
Rais Samia Suluhu Hassan hakika ameupiga mwingi hapa nchini kwa kazi
kubwa aliyoifanya ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Alisema
Rais Samia hakuna sehemu aliyoiacha bila ya kuifikia kwa maendelea
katika sekta zote na ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza nchi ambapo
aliwaomba watanzania kuendelea kumuombea kwa Mungu na kuunga mkono
jitihada zakezote za maendeleo anazozifanya.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Singida Mjini Lusia Mwiru alimpongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha mwaka mmoja
ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM wenye sifa ya kugombea
nafasi mbalimbali kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi
wa ndani utaofanyika hivi karibuni.
Wenyeviti wa Halmashauri za wilaya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Ally Mwanga (Ikungi), Innocent Msengi (Iramba) na Eliya Digha Singida DC.
Viongozi wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Stamili Dendegu, Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Singida, Asha Stambuli na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Singida, Vaileth Soka.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Makatibu wa CCM wa Wilaya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakiwa kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wake.
Hafla ikiendelea.
Katika hafla hiyohiyo kila wilaya mkoani hapa ilitoa taarifa ya fedha walizopokea kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo walioifanya ambayo ziliwasilishwa na Wenyeviti wa Halmashauri husika ambapo katika Wlaya ya Ikungi Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ally Mwanga alisema walipokea Sh.11,263,030,397 ambazo zilitumika katika Elimu, Afya, Utawala, Mfuko wa Jimbo, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi alisema wao walipokea Sh.10,960,988,976 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo huku Wilaya ya Itigi wakipokea Sh.7,435,318,522 na Manyoni Sh.10,505,419,366.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama walipokea Sh.7,811,623,781, Singida DC Sh.10,046,768,035, Singida Manispaa Sh.5,791,791,192, Sekretarieti ya Mkoa Sh.875,552,414, Tanesco Sh.63,507,622,522, jumla kuu ikiwa ni Sh.128,198,115,205.