Elimu ya UVIKO-19 yatajwa kuwa na mchango mkubwa mwitikio wa chanjo

NA DOREEN ALOYCE

IMEELEZWA kuwa uwepo wa elimu juu ya chanjo ya UVIKO-19 inayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyokuwa na kiserikali hapa nchini imesaidia wananchi kujitokeza na mwitikio mkubwa kupata chanjo hiyo tofauti na hapo awali ilipoanza kutolewa.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma za afya ya jamii,elimu na maendeleo la STEPS TANZANIA, Dkt. Cyprian Magere wakati alipokuwa kwenye kikao kazi cha kutathimini Afua ya Kifua Kikuu na ugonjwa wa UVIKO-19.

Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya na asasi mbalimbali za kijamii ukiwemo Mkoa wa Dodoma na Simiyu ambao wamefanikiwa juu ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na kuibua wagonjwa wa kifua kikuu TB.

Aidha, Dkt.Magere amesema kuwa katika kutoa mafunzo hayo ambayo yanafadhiliwa WFP tayari wamefikia watoa huduma ya afya ya msingi 289 Mkoa wa Dodoma ambao wameshapewa elimu hiyo.
"Hii ilitokana na hofu ya wananchi waliyokuwa nayo ambapo walikimbia na wengine kuwa na woga juu ya chanjo ya UVIKO-19, lakini baada ya kuwapa elimu wa huduma walirudi na mikakati ya kuwaibua wagonjwa wapya na kuwarudisha huku wakitoa elimu jambo ambalo lilileta mafanikio ambapo kumekuwa na ongezeko,"amesema.

Amesema, Steps Tanzania Bado inaendelea na juhudi za kutoa elimu kwa watoa huduma ngazi ya jamii jambo ambalo litaendelea kisaidia kuwa na uelewa zaidi.
Mratibu wa chanjo Mkoa wa Dodoma, Dkt.Francis Bujiku amesema, kwa Mkoa wa Dodoma mwitikio wa wananchi ni mkubwa kwani tayari wamefikia asilimia nzuri tangu kuanze kutolewa chanjo hiyo.

"Tunapaswa kuwafikia wananchi wa Dodoma kwa asilimia 60 ndani ya miezi hii miwili tumetoka asilimia 6.3 na mpaka takwimu za jana kwa waliokingwa ni asilimia kumi na kwa hapa Tanzania ni mikoa michache imefikia asilimia hiyo,"amesema Dkt. Bujiku.
Nae mshiriki wa kikao hicho kutoka shirika la mwitikio wa kifua kikuu na ukimwi Tanzania (MKUTA), Juliana Mollel amesema Shirika la Steps Tanzania limeonesha mfano bora katika kuhamasisha jamii.

"Nafurahi sana kuona shirika hili ni hatua nzuri ya afua kisha kurudi kufanya tathimini ya jinsi gani umefanikiwa na kuangalia tija iliyopatikana hali hiyo inasaidia kuongeza namba,"amesema Mollel.

Kwa upande wao wakazi wa jiji la Dodoma wamesema chanjo ya UVIKO-19 inapaswa kuendelea kupewa kipaumbele hasa kuhusu elimu kutolewa kwenye jamii ili Taifa liendelee kuwa katika hali ya usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news