NA FRESHA KINASA
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara, Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi anatarajia kuhitimisha mashindano ya Mathayo Cup 2022 kwa watumishi wa Serikali na mashirika ya umma siku ya Jumapili ya Aprili 3, 2022 katika Uwanja wa Posta uliopo Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara.

Aidha, pambano la fainali litawakutanisha Kati ya RAS-MARA V/S MASHTAKA (NPS) majira ya saa 04:00 za jioni hadi saa 06:00 jioni ambapo Mheshimiwa Mbunge Vedastus Mathayo Manyinyi atashuhudia mchezo huo akiwa ameambatana na Waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Musoma.
Wananchi wa Jimbo la Musoma Mjini na Mkoa wa Mara kwa ujumla wameombwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani michezo ni furaha, amani, ajira na pia ni fursa ya ajira na kuimarisha afya sambamba na kudumisha mahusiano mema katika jamii na Taifa pia.

"Mheshimiwa Mathayo amekuwa akishirikiana na wananchi wa Jimbo la Musoma Mjini wakati wote, amekuwa akifanya ziara za kutembelea kila mtaa na kata kusikiliza changamoto na kuzipatia ufumbuzi papo kwa hapo.
