Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Machi 6, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa benki kuwekeza katika viwanja mbalimbali vilivyopo katika balozi nje ya nchi, huku akimpa jukumu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela Kuhamasisha wenzake kufanya hivyo.

Rais Samia amesema hayo Machi 5, 2022 katika uzinduzi wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

“Naomba niwadokeze kipengele kingine ambacho mnaweza kuwekeza, jana tulikuwa na mkutano wa bajeti, tulijadili bajeti yetu lakini tukakuta kwenye Wizara ya Mambo ya Nje kuna viwanja vingi vipo nje ya nchi ambavyo ni mali yetu.

“Lakini kama Serikali yetu inashindwa kuvijenga, naomba tumieni hiyo kama fursa ya uwekezaji, nendeni mkajenge majengo mkodishe, mfanye biashara zenu ili viwanja vile tusiendelee kunyang’anywa.

“Kwa sababu tunanyang’anywa tunasikitika tunarudishiwa, tunanyang’anywa tena, bado havijengwi, kuna viwanja vina miaka 20, 15 bado havijajengwa, naomba sana wewe Abdulmajid ni Mwenyekiti wa wenzio naomba uwaunganishe, uwaratibu muitimue hii fursa jinsi itakavyowezekana,"amesema Rais Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news