>Yasaini mikataba 57 na Wazabuni
NA IRENE THOMSON
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili (MNH) imepongezwa kwa hatua ilizofikia katika
utekelezaji wa miradi ya afya kutokana na fedha za UVIK0-19 ambapo hadi
sasa imesaini mikataba 57 na wazabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba
mbalimbali.Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (hawapo pichani) wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za Uviko-19.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Prof. Abel
Makubi alipotembelea MNH ili kukagua utekelezaji wa miradi ya fedha za
UVIKO-19 ambapo kiasi cha fedha shilingi Bilioni 25,540,868,000 zilizopokelewa
hospitalini hapo kwa ajili ya miradi ya MNH na kupewa jukumu la kununua
vifaa vya Hospitali za Rufaa za Mkoa Amana, Temeke, Mwananyamala na
Tumbi.
Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema kati ya fedha hizo, MNH
ilipangiwa shilingi bilioni 11,876,800,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba
kama MRI, CT-Scan, Angio suite, vifaa vya ICU, ujenzi na ukarabati wa
idara ya magonjwa ya dharura na kitengo cha dharura kwa kina mama
wajawazito na nyinginezo. Hadi sasa MNH imesaini mikataba 16 na wazabuni yenye
thamani ya shilingi bilioni 11,874,740,103.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na fedha za Uviko-19.
Prof. Museru amesema, Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke
ilipangiwa shilingi bilioni 4,071,470,000 kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital
X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya
magonjwa ya dharura n.k. Hadi sasa Temeke imesaini mikataba 11 na
wazabuni yenye thamani ya shilingi 3,559,365,995.84.
Hospitali ya
Rufaa Mkoa wa Amana ilipangiwa shilingi bilioni 4,065,490,000 kwa ajili ununuzi
wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU,
radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura na nyinginezo.
"Hadi sasa Amana
imesaini mikataba tisa na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 3,586,829,769,"amesema Prof. Museru.
Wajumbe wa Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kulia) wakielekea kukagua miradi ya maendeleo.
Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mwananyamala, Prof. Museru
amesema kuwa, ilipangiwa shilingi bilioni 1,889,490,000 kwa ajili ununuzi wa
Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya
idara ya magonjwa ya dharura na vinginevyo. Hadi sasa Mwananyamala imesaini
mikataba 10 na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 1,708,103,228.20.
Hospitali
ya Rufaa Mkoa wa Tumbi ilipangiwa shilingi bilioni 3,641,554,000 kwa ajili
ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU,
radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura na nyinginezo. "Hadi sasa Tumbi
imesaini mikataba 11 na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 3,530,686,314.96,"amesema Prof. Museru.
Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Muhimbili, Mhandisi Gaudence Aksante (kushoto) akitoa maelezo kwa katibu mkuu kuhusu maendeleo ya mradi mmojawapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi akikagua maendeleo ya ukarabati wa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU).
Kutokana na maelezo hayo, Prof. Makubi ameonesha kuridhika na taarifa ya Prof. Museru na kuongeza hizi ni dalili za moja kwa moja kwamba utekelezaji wa miradi utakamilika ndani ya muda husika ambao ni Aprili mwaka huu.
“Kasi ya utekelezaji wa miradi inaridhisha nina matumaini makubwa kuwa miradi hii itakamilika ndani ya muda tuliojiwekea na hata kama muda utazidi nina imani haitakuwa zaidi ya wiki ya kwanza ya mwezi Mei, hivyo nawapongeza sana kwa hatua hii muhimu,”amesema Prof. Makubi.