HWPL:Uvamizi wa kijeshi dhidi ya Taifa huru hauwezi kuwa suluhisho la tatizo lolote

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SEHEMU nyingi za jamii ya Kimataifa zimejibu kuhusu uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine kwa kukataa uamuzi wa Rais Vladimir Putin wa Urusi wa kushambulia na kuvamia eneo la Ukraine.
Katikati mwa jiji la Kharkiv nchini Ukraine pakiwaka moto baada ya shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa Urusi Machi 2, 2022. (Picha na State Service of Ukraine for Emergencies).

Katika urais wake, Putin alitumia nguvu za kijeshi kuvamia na kudhibiti eneo la kigeni ikiwa ni pamoja na Ossetia Kusini, Crimea ya Ukraine, na sasa sehemu za Kaskazini, Mashariki na Kusini mwa Ukraine, ambazo zote zilimehatarisha usalama na utulivu wa ulimwengu.

Mnamo tarehe 28,2022 Utamaduni wa Mbinguni, Amani ya Dunia, Marejesho ya Mwanga (HWPL), NGOs ya Kimataifa ya Korea Kusini yenye uhusiano na Serikali ya Umoja wa Mataifa ya ECOSOC na Seoul Metropolitan, ilitoa taarifa ya kutetea ushirikiano wa kimataifa kwa amani.
Roketi ya Urusi ambayo inadaiwa iligonga jengo la makazi huko Kyiv Februari 26, 2022. (Picha na Eyewitnesses from Social Networks).

Ni taarifa iliyopewa jina la "Taarifa ya Utamaduni wa Mbinguni, Amani ya Dunia, Urejesho wa Nuru (HWPL) Kuhusu Urusi na Ukraine", inaitaka Urusi iondoe jeshi lote katika eneo lake, jumuiya ya kimataifa kulinda na kuwapa nafasi wakimbizi, na vijana wa kimataifa kuungana kwa harakati za kupambana na vita na amani.

"Uvamizi wa kijeshi dhidi ya taifa huru hauwezi kuwa suluhisho la tatizo lolote, na hatari ya vita hivyo na migogoro ya vurugu inawapiga raia wasio na hatia kwa nguvu zaidi, ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana, na watoto...Urusi inapaswata kuondoa vikosi vyake nchini Ukraine, na sisi tunaomba mataifa yote kuonesha upendo wao kwa ubinadamu, kwa kutoa msaada kwa wakimbizi,"imeeleza taarifa hiyo.
Wanajeshi wa Urusi siku ya Machi Mosi, 2022 wanadaiwa walirusha kombora katika mnara wa TV huko Kyiv nchini Ukraine. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine).
 
HWPL imekuwa ikitafuta kujenga mtandao wa kimataifa wa amani kwa kujenga mshikamano miongoni mwa viongozi na wawakilishi kutoka nyanja za siasa, dini, vijana, wanawake na vyombo vya habari duniani. 

HWPL mnamo 2018 ilituma "barua za amani" ikiwataka wakuu wa nchi 192 kudai ushiriki wao katika ushirikiano kwa amani, barua hizo zimeandikwa na wananchi 580,000 duniani kote.

Mnamo Februari 26, White House ilitangaza kupitia waraka kwamba Tume ya Ulaya, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza, Canada na Marekani itashirikiana kutekeleza vikwazo vya kiuchumi ili kuitenga Urusi kutoka kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa kwa kuondoa benki za Urusi zilizochaguliwa kutoka SWIFT.

Vikosi vya Ukraine kwa sasa vinapinga jeshi la Urusi kwa ulinzi madhubuti, na maandamano ya kupinga vita na sauti za kuunga mkono Ukraine kupitia vyombo vya habari vya kijamii vinaenea zaidi duniani kote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news