KMC FC:Tuna jambo letu dhidi ya Yanga SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MARA baada ya kumalizika kwa mapumziko ya siku moja kikosi cha KMC FC leo kimeanza tena maandalizi ya kujiandaa na mchezo mwingine wa 18 wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Machi 19, 2022 katika Uwanja wa BenjaminiMkapa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC,Christina Mwagala ambapo amefafanua kuwa,katika mchezo huo muhimu timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itakuwa ugenini ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguko wa 17 dhidi ya Coastal Union.
Mchezo uliopigwa siku ya Jumatatu ya Machi 7,2022 katika uwanja wa Azam Complex na kupoteza kwa mabao matatu kwa mawili.

KMC FC imesaliwa na siku nane za kujiandaa na mchezo huo na katika kipindi hiki Kocha Mkuu Hitimana ameandaa programu ya mazoezi mbalimbali.

Sambamba na kucheza mechi za kirafiki ambazo zitakuwa muhimu kwa ajili ya kuwaweka wachezaji katika hali nzuri.

Katika maandalizi hayo, KMC FC inafahamu kuwa inakwenda kucheza na timu ambayo inaongoza ligi kwa sasa na kwamba kila mmoja anatambua,ugumu na ushindani utakaokuwepo katika mchezo huo lakini hiyo haitazuia Kino Boys kupata matokeo mazuri kutokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo.
“Tunakwenda kwenye mchezo muhimu ambao kimsingi tunafahamu utakuwa na ushindani mkubwa, lakini pamoja na ushindani huo haimanishi kuwa KMC tutashindwa kupata matokeo, kimsingi kila mmoja anahitaji ushindi na kila siku tumekuwa na maandalizi bora kwa kila mchezo ambao unakuwa mbele yetu.

"Ukiangalia ratiba ya mchezo wetu ni Machi 19,kwa hiyo tunakaribu siku nane za kufanya maandalizi yetu, kikubwa ni kujipanga vizuri, kuzitumia vizuri siku hizi za mazoezi, tunaamini kuwa tutakuwa bora kwenye mchezo huo na hivyo kufanya vizuri kutokana na ubora wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji tuliliokuwa nao.

KMC FC kwa sasa ipo katika nafasi ya sita ikiwa imecheza michezo 17 na kushinda michezo mitano, sare michezo saba huku ikipoteza michezo mitano na hivyo kukusanya jumla ya alama 22 muhimu na kwamba bado inahitaji kupanda zaidi kwenye nafasi tatu za juu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news