LAAC yatoa maelekezo kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Sanjo

NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Selemani Zedi ameushauri uongozi wa Shule ya Sekondari Sanjo kuendelea kushirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo ya elimu katika maeneo wanayoishi.
Mhe. Zedi ametoa wito huo Machi 21, 2022 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambapo walikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Jengo la Utawala na Shule ya Sekondari Sanjo iliyopo Kata ya Usagara na kuridhishwa na miradi iliyokuwa inaendelea na ujenzi katika halmashauri hiyo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara vilivyokamilika vikiwemo na vifaa vya kujifunzia, Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Emmanuel Kulwa amesema, mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ulipokea fedha kutoka Serikali Kuu shilingi milioni 60 na shilingi milioni 54 ni nguvu ya wananchi.
Amefafanua kuwa, lengo la mradi wa ujenzi wa maabara ni kuongeza ufaulu wa masomo ya sayansi ambapo hapo vifaa vya maabara vilikuwa vikihifadhiwa stoo na wakati wa kujifunza vifaa hivyo huhamishiwa darasani hali iliyopelekea kuwa na mazingira magumu ya kufundisha na kujifunzia na wakati mwengine vifaa hivyo huaribika kwa sababu ya kuvihamisha kila mara. 

“Mwaka 2021 watahiniwa wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi ni 301 watoto 64 walifaulu vizuri asilimia 100,"amesema Mwalimu Kulwa.

Ameongeza kuwa, kukamilika kwa maabara hiyo kumesaidia kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi, lakini pia wanafunzi hao kwa sasa wanajifunza kwa nadharia na vitendo, lakini pia uharibifu wa vifaa umepungua kwa sababu vimewekwa sehemu salama,”amesema Mwalimu Kulwa.

Mhe.Zedi ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari Sanjo na kutoa wito kwa walimu kutumia maabara hiyo kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi ili Taifa liwe na wataalam wakutosha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news