LAAC yatoa tiki ujenzi jengo la utawala Halmashauri ya Mbeya

NA MWANDISHI MAALUM, OR-TAMISEMI

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Pia imemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Stephene Katemba kuendelea kusimamia na kufanya tahmini ya matumizi ya fedha katika kila hatua ya utekelezaji.
Akizungumza Machi 21, 2022 Kaimu Mwenyekiti, Mhe. Boniface Butondo amesema, baada ya kukagua ujenzi huo kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha ukilinganisha na hatua ya utekelezaji iliyofikiwa.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe.Butondo amewashukuru wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kushiriki katika uchimbaji wa msingi hatua ambayo imeokoa sh. milioni 1.7.

"Niwashukuru wananchi kwa kuchangia nguvu kazi na niwaombe muendelee na ari hiyo kwa miradi mingine ya maendeleo ili kupunguza gharama za ujenzi,"amesema.

Kwa upande wake, Mhe.Francis Mtinga mbaye ni mjumbe wa kamati amempongeza Mkurugenzi kwa kununua mashine kwa ajili ya kufyatulia tofali na mashine ya kuchanganyia zege vifaa ambavyo vitasaidia kupungiza gharama za miradi na zitatumia kwa miradi mingine ya maendeleo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bw.Stephene Katemba amesema hadi kukamilika ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya utagharimu kiasi cha sh. bilioni 2,792,073,029.88 kati ya hizo sh.bilioni 2,700,000,000 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu na sh.milioni 92,073,029.88 zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa jengo ambao umelenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news