MAENDELEO YALIYOFIKIWA KATIKA UFILISI WA ILIYOKUWA BENKI YA FBME LTD


Taarifa inatolewa kwa wateja na wadau wote wa iliyokuwa FBME Bank LTD kwamba, Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imetengeneza mfumo wa taarifa (DIB Portal) kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na wadau na kubadilishana taarifa juu ya ufilisi wa benki hiyo;

Kwa taarifa hii, DIB inawaalika wenye amana, wadai na wadau wote wenye madai dhidi ya benki ya FBME kufanya maulizo na kutoa maoni yao kuhusu ufilisi wa benki hiyo kupitia mfumo huo wa taarifa unaopatikana katika tovuti ya DIB: www.dib.go.tz na tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania: www.bot.go.tz. Ili kupata taarifa, tafadhali jaza fomu inayopatikana kwenye tovuti ya DIB ambapo msimamizi wa mfumo atakupatia namba ya ruhusa na kukuwezesha kuzifikia taarifa mbalimbali zilizopo kwenye mfumo huo.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news