NA MWANDISHI WETU
KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Mwakilema amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo hivi karibuni.


Kamishna Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake ameahidi ushirikiano kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya shirika.
Kamishna Mwakilema amewataka makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele katika majukumu yake ya uhifadhi.

"Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye,"amesema Kamishna Mwakilema.
