Mama Maryam Mwinyi awapa tabasamu wanawake, watoto Zanzibar

Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Dkt. Mwatima Abdalla Juma akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya wasichana Ben Bella Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi wakati walipofika skulini hapo kwaajili ya kuwapaTia msaada wa taulo za kike wanafunzi wa Skuli hiyo. Maryam Hashim Abdalla mgonjwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital ya maradhi ya akili kidongo Chekundu akitoa neno la shukurani Kwa niaba ya wagonjwa wenziwe mara baada ya kupokea msaada wa taula za kike kutoka ZMBF chini ya Mwenyekiti wake mama Maryam Mwinyi . Mjumbe wa Bodi ya Zanzibar maisha Bora Foundation (ZMBF), Dkt.Mwatima Abdalla Juma Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi akiwakabidhi Watendaji katika nyumba ya kulelea watoto yatima mazizini boksi la taulo zakike ikiwa nimsaada kutoka ZMBF kwa ajili ya watoto wakike wanaishi katika nyumba hiyo. Mtoto Faizuni Joseph Lumelezi wa nyumba ya kulelea watoto yatima mazizini akitoa neno la shukurani mara baada ya kupokea msaada wa taula za kike na pempas Kwa ajili ya watoto hao kutoka kwa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation chini ya Mwenyekiti wake mama Maryam Mwinyi. Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),Dkt.Mwatima Abdalla Juma akizumgumza na watendaji wa Hospitali ya KMKM wakati alipofika Hospitalini hapo kwa niaba ya Mwenyekiti wa (ZMBF) ambae pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi kutoa msaada wa Pempas kwa watoto wanaozaliwa Hospitalini hapo,wakwanza kulia ni Mkuu wa Kikosi cha KMKM Komodoo Azana Msingiri .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news