NA MARY MARGWE
WADAU mbalimbali mkoani Manyara wameitumia Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2022 kupanda miti katika Shule ya Msingi Orkesumet, ambapo kimkoa ilifanyika wilayani Simanjiro mkoani humo.
Kwa
Tanzania maadhimisho hayo ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Arusha yameongozwa na kaulimbiu isemayo “Kizazi cha
haki na usawa kwa maendeleo endelevu, tujitokeze kuhesabiwa”.
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula akiwaongoza viongozi mbalimbali kupanda miti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika kimkoa wilayani Simanjiro mkoani Manyara. (Picha na Mary Margwe).
Mrakibu wa Polisi Wilaya ya Simanjiro, SP Christina Mkonongo akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Orkesument kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula alikuwa ndiye mgeni rasmi huku akiwaongoza viongozi mbalimbali kupanda miti kwenye maadhimisho hayo.(Picha na Mary Margwe).

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Sendeu Laizer baada ya kupanda mti wake wa kumbukumbu. (Picha na Mary Margwe).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Samwel Warioba akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Orkesument kwenye Siku ya Wanawake Duniani ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula alikuwa ndiye mgeni rasmi huku akiwaongoza viongozi mbalimbali kupanda miti kwenye maadhimisho hayo.(Picha na Mary Margwe).
Mkuu wa Wilaya Simanjiro mkoani Manyara, Dkt.Suleiman Serera akipanda mti katika Shule ya Msingi Orkesument kwenye Siku ya Wanawake Duniani ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula alikuwa ndiye mgeni rasmi huku akiwaongoza viongozi mbalimbali kupanda miti kwenye maadhimisho hayo.(Picha na Mary Margwe).