Mbunge Aesh Hilary ataka vyanzo vya maji viheshimiwe

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Sumbawanga, Aesh Hilary amewashauri wakazi wa Kata ya Milanzi mjini Sumbawanga kuacha shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ili waepuke tatizo la kutumia maji machafu sambamba na magonjwa mbalimbali yanayowasumbua.
Ushauri huo ameutoa wakati akihutubia wakazi wa Kijiji cha Matanga alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara ambapo wananchi hao walilalamikia kuugua magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa njia ya mkojo (U.T.I) pamoja na magonjwa ya tumbo.

Amesema kuwa, wamekuwa wakilalamika, lakini wapo baadhi ya wananchi wenzao wanalima, kupita pamoja na kuchungia mifugo karibu na vyanzo vya maji, vitendo ambavyo ni hatari kwa afya zao.

Mbunge Hilary amesema kuwa, ili waepukane na changamoto hizo ni lazima Serikali za vijiji zitumie sheria za mazingira ili ziwabane watu hao kwani ndio chanzo cha matatizo yao na hakuna njia nyingine ya kufanya tofauti na hiyo.

''Ninyi mnalalamika, mnatumia maji machafu, lakini baadhi yenu wanalima na kunywesha maji mifugo yao kwenye vyanzo vya maji mnayotumia, lazima ya chafuke na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kuugua magonjwa yanayo wasumbua,"amesema.

Naye Janeth Sadala mkazi wa kata hiyo aliishukuru serikali kwa ujenzi wa kituo cha afya unaoendelea katika kijiji cha Matanga kata hiyo kwani kitawasaidia wajawazito na watoto wanaolazimika kusafiri umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma za afya.

Alisema kuwa, kwa miaka mingi wamekuwa wakisubiri kutimia kwa ahadi hiyo ya ujenzi wa kituo cha afya, na sasa Serikali ya Awamu ya Sita imeitekeleza na pia alimshukuru Rais Samia Hassan kwani anajua adha wanazokumbana nazo wakina mama ndiyo maana ametoa fedha za ujezi wa kituo hicho cha afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news