Mheshimiwa Kipanga akagua maendeleo ya Awamu ya Pili ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Elimu eneo la Mtumba jijini Dodoma

NA MWANDISHI MAALUM-WyEST

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Kipanga (Mb) amekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Dodoma kwa kukagua maendeleo ya awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la ofisi za wizara hiyo iliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Kipanga (Mb) akikagua eneo litakapojengwa jengo la Wizara huku akiwa ameambatana na baadhi ya watumishi wa Wizara, Mkandarasi na Mshauri elekezi. Jengo hilo linalojengwa eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Kipanga (Mb) akifafanua jambo kwa mkandarasi, Li Yang na Mshauri elekezi, Anania Saudeni wakati alipokuwa akikagua eneo litakapojengwa jengo la Wizara lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa sehemu ya eneo linapojengwa jengo la Wizara ya Elimu lililopo Mtumba jijini Dodoma

Mhe. Kipanga ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi na kumtaka mkandarasi wa ujenzi huo, kampuni ya CRJE (EA) Limited kuhakikisha wanatekeleza ujenzi huo kwa kiwango na kukamilisha kwa wakati uliopangwa.

Aidha, amefafanua kuwa ujenzi wa jengo hilo utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 15.9 na kwamba jengo litakuwa na sakafu nane ikiwemo sakafu ya ardhini (basement), sakafu ya chini (ground floor) na sakafu za juu sita.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Kipanga (Mb) akiongea na baadhi ya watumishi wa Wizara, mkandarasi na mshauri elekezi kabla ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Wizara hiyo linalojengwa eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Akitoa ripoti ya mradi huo, Mkadiriaji Majenzi kutoka Chuo cha Ardhi ambao ndio wasimamizi elekezi wa Mradi, Anania Saudeni amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza Desemba 2021 na unatarajia kukamilika Desemba 2023 na kwamba mpaka sasa umefikia asilimia tano.

Naye Meneja wa Mradi huo, Li Yang ameihakikishia Wizara hiyo kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango kinachotarajiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news