Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete: Serikali ya Rais Samia ukiipibu kwenye maendeleo inakupigia,tutekeleze majukumu yetu na kutoa taarifa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE wa Chalinze mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ukiiambia unataka madarasa mawili au matatu yote inakuletea kwa sababu imekuwa na usikivu na kasi kubwa sana ya kupeleka fedha za maendeleo kwa wananchi.
Mhe. Ridhiwani akitolea mfano kwenye Jimbo la Chalinze amesema, wao mwaka jana waliomba madarasa kwenye Shule za Msingi na Shule Shikizi lakini wakachomekea tu na madarasa kwa Shule za Sekondari lakini Serikali ya Rais Samia ikaleta fedha kwa ajili ya madarasa ya Shule za Msingi na Shikizi mpaka madarasa ya Sekondari.

Mhe. Ridhiwani amesema hayo wakati akifanya Mkutano Kijiji cha Kwa- Msanja, Kata ya Kibindu, Machi 6, 2022 wakati wa mwendelezo wa ziara yake kwenye Jimbo lake la Chalinze akisikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akiwaeleza pia na mipango mikubwa ya maendeleo inayokuja kwa wananchi kwenye maeneo yao kutoka ngazi ya halmashauri mpaka Taifa.

Pia akatumia mkutano huo kusisitiza Uongozi wa Vijiji, Kata na Halmashauri kupata tathmini ya taarifa ya kero zilizopo na upungufu kwenye maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kwa Wananchi ili inapoombwa bajeti ya maendeleo lisisahaulike jambo na fedha ipatikane ya kutosha huku akiwataka watumishi kuhakikisha kero zote zilizotolewa na wananchi kwenye mikutano yake ziwe zinatekelezwa.

Katika hatua nyingine, kuhusu kero za uchakavu wa madarasa na nyumba za Walimu, changamoto ya mawasiliano, kituo cha Polisi kutoisha zote zikajibiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Mhe. Posi ambaye alieleza ofisi yake kuanzia Jumatatu itatuma Wataalamu kufanya tathmini ya changamoto ili haraka fedha ipelekwe kwa ajili ya kumaliza changamoto hasa ya uchakavu wa nyumba za Walimu, madarasa, umaliziaji wa Kituo cha Polisi Kwa- Mduma na zingine zikichukuliwa kwa ajili ya kusukumwa zaidi juu kwa ajili ya utekelezaji kama lile suala la changamoto ya mawasiliano.

Suala la maji pia linakwenda kuwa historia ambapo katika eneo la Kwa- Msanja panajengwa Bwawa kubwa la Maji ambalo litahudumia wakazi wa maeneo yote yanayozunguka Kwa- Msanja huku suala la umeme likiwekewa utekelezaji kufikia Bajeti ya Mwaka unaofika maeneo yote ya Vitongoji Kwa- Msanja, Kwa- Mduma na Kwa- Konje ambayo hayajafikiwa na umeme yatafikiwa.

Suala la tembo kuvamia mashamba ya Wakulima nalo likatolewa majibu kwamba na Mkurugenzi kwamba tayali risasi zimenunuliwa ili kusaidia kupambana na tembo hao kuwaondoa maeneo yenye shughuli za watu.

Mhe. Ridhiwani kwenye maeneo yote aliyopita ameendelea pia kuwasisitiza Wananchi kufuata sheria ya kuchunga na mambo ya ardhi ili kuondoa migogoro mbalimbali inayoendelea huku ile iliyopo ya Kati ya Vijiji na Vijiji au Hifadhi na mtu kwa mtu, yote ikiwekewa mipango ya kutatuliwa.

Kwenye ziara hii ya Mhe. Mbunge na Naibu Waziri anayoifanya kwenye Kata mbalimbali, ameambatana na Wataalamu wote wa Halmashauri ya Chalinze ambao wamekuwa wakitolea ufafanuzi wa kero mbalimbali na mipango ya Halmashauri ya maendeleo kwa Wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news