Mradi wa DADPs kuzinufaisha halmashauri 30 nchini

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI imezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe zinafuata utaratibu uliopangwa katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dodoma wakati akiongea na wataalam wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Kilimo na wadau kutoka Alliance for a Green Revolution in Africa-AGRA.

Waziri Bashungwa amesema, Mpango wa Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) utasaidia kuongeza uzalishaji na kuongeza mapato lakini pia amesema kwa mwananchi utasaidia kuwa na malengo katika kufanya shughuli za uzalishaji wenye kuleta tija.

Aidha, uratibu wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa “Strengthening Coordination of ASDP II at Local Government Authorities (SCALGA) Waziri Bashungwa amesema, ili kuwezesha halmashuari zetu kuweza kufanya kazi za kilimo katika kuongeza uchumi wa nchi na kwa mwananchi anazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutotumia tofauti maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.

"Pia nawaelekeza Maafisa Ugani ambao nyie ndio wataalam mlioko huko msimamie kazi zenu na ukiwemo huu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo, huu mpango ni sekta ya uvuvi, kilimo na mifugo muhakikishe wananchi wetu wanafanya shughuli zao za uzalishaji na wananufaika nazo,"amesema.

“Huu mpango umetupa muongozo, mradi huu ni wa awamu ya pili sasa nitoe wito kwa viongozi wenzangu ukianza kutekelezwa tukausimamie ili wananchi tunaoenda kuwasimamia wanakuwa na maslahi nao,”amesisitiza Mhe. Bashungwa.

Amesema kuwa, Serikali inatambua kila halmashauri ina mpango wake ila Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP) utaanza kutekelezwa katika Mikoa 12 na Halmashauri 30 Kagera (Muleba, Misenyi na Biharamulo), Kigoma (Kasulu, Kibondo na Kakonko), Katavi (Tanganyika, Mpimbwe na Nsimbo).

Rukwa (Kalambo, Nkasi, Sumbawanga DC), Ruvuma (Songea DC, Madaba na Mbinga DC), Njombe (Wanging’mbe, Ludewa), Iringa (Mufindi, Kilolo), Manyara (Babati, Hanang na Kiteto), Arusha (Meru, Karatu na Arusha DC), Kilimanjaro (Hai, Siha na Rombo), Simiyu (Maswa) na Tanga (Kilindi).

Mpango wa Mradi wa “District Agriculture Development Plan” (DADPs) ulizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa tarehe 3 Machi, 2022 jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news