Mwalimu atakayebainika kudai malipo kwa wanafunzi atachukuliwa hatua za kisheria-RC Mjema

NA KADAMA MALUNDE

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria walimu watakaobainika kudai malipo kwa wanafunzi akisema elimu ni bure.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. (Picha zote na Malunde 1 Blog).

Mjema ametoa agizo hilo Machi 3,2022 akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.

“Kumekuwa na upotoshaji huko mtaani kuwa wazazi wanatakiwa kulipa ada. Napenda kusisitiza kuwa elimu ni bure,hakuna malipo, mwalimu yeyote atakayebainika kuchangisha fedha achukuliwe hatua. Tutaendelea kutatua changamoto zilizopo ikiwemo utoro,chakula, upungufu wa walimu,nyumba za walimu.

“Tunachokwenda kufanya sasa ni kuboresha mazingira yaliyopo shuleni. Wote tunatakiwa tushikamane, upande wa shule binafsi na za serikali. Tunataka shule zetu ziingie kumi bora kitaifa kila mwaka.Walimu na wadau wote tuwe wabunifu, wakurugenzi tuwe na ubunifu pia kwa kuwapa motisha walimu ikiwemo kuwapatia nyumba, mtaona hawataondoka, hawatakimbia na ufaulu utaongezeka.

"Waheshimiwa Ma DC (Wakuu wa wilaya) nendeni mkasimamie upatikanaji wa chakula shuleni, Tunataka lishe bora shuleni ili watoto wakue vizuri. Tukasimamie pia mdondoko, watoto wafuatiliwe wako wapi, watoto wanatakiwa wawe shule kama tulivyowaandikisha, tusikubali kuwa chini ya asilimia 100,”amesema Mjema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dafroza Ndalichako akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa (kushoto) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko wakisoma nyaraka kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news