Mzee Mrema: Doreen ni wangu, endeleeni kupoteza muda mitandaoni kujadili ndoa yetu, sisi wala hatujali

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama cha TLP Taifa, Augustine Lyatonga Mrema amesema anamshukuru Mungu kwa sherehe ya ndoa yao kwenda vizuri na kwamba wanaoendelea kueneza uzushi na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii wanapoteza muda wao.
Pia amesema, anamshukuru Mungu kwa sababu taratibu zote za ndoa zilifuatwa, hivyo mke wake Doreen Kimbi hajamuoa kinyemela.

Mzee Mrema amesema, ndoa yake ilikuwa ifanyike Machi 8, mwaka huu lakini waliamua kuisogeza mbele hadi Machi 24, mwaka huu ili kutoa fursa kama kulikuwa na mtu ambaye angejitokeza kuweka pingamizi ndoa isiweze kufungwa.

"Ndoa imetangazwa kanisani mara tatu na hakuna mtu yeyote aliyejiyokeza kusema Doreen alikuwa mke wangu, kwa hiyo uvumi wa mitandaoni hauna maana yeyote na wanaofanya hivyo wanadhani watavuruga ndoa yetu kumbe wanapoteza muda wao bure," amesema Mrema.

Amesema, hadi kufikia Machi 23, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya kufungwa kwa ndoa hiyo hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kutoa pingamizi, hivyo wanaoeneza uvumi mbalimbali kwenye mitandao wanapoteza muda wao na ndoa imeshafungwa na hivyo suala hilo limeshapita.

Mrema amesema, uvumi wa mambo yote hayo unatokana na kwamba watu hawajazoea mtu akipendwa kwa dhati na mtu mwingine,watu wamezoea rushwa wanahonga watu,wananunua watu,kwa hiyo wanafikiri kila mtu ananunulika.

Amesema, mara baada ya mke wake kufariki Septemba, mwaka jana, alimuacha katika mazingira magumu sana hivyo alimuomba Mungu amsaidie ili apate msaidizi mwingine.

"Mke wangu alipofariki aliniacha katika mazingira magumu sana, afya ilikuwa imedorora hata hotuba yangu wakati wa kumzika sikuweza kusimama, nilimuomba Mungu na mke wangu atakapokuwa anisaidie nipate mtu atakayenitunza, atakayeniangalia," amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news