Namba za taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na zile za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizounganishwa kupitia mfumo wa Sema na Rais Mwinyi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI ya Awamu ya Nane ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi inasimamia mfumo wa kielekroniki ambao unawezesha kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kueleza changamoto wanazopitia wanapokwenda kuhudumiwa katika taasisi za serikali.

Mfumo huo uliopewa jina la “Sema na Rais Mwinyi (SNR)” unawezesha wananchi kupiga simu au kutuma ujumbe kwa njia ya tovuti.

Aidha, mlalamikaji anaweza kuambatanisha hati, sauti na hata picha kama ushahidi wakati wa kuwasilisha malalamiko kisha mlalamikaji atapokea namba ya siri ili kufuatilia kujua lalamiko lililotolewa limefika wapi kupata ufafanuzi na afisa anayeshugulikia.

Rais Mwinyi anasema mfumo huo ni moja ya utekelezaji wa ahadi zake kipindi cha kampeni, “Baada ya kuwasikiliza Wazanzibari nilitoa ahadi ya kuwa karibu yenu kwa kusikiliza na kutatua changamoto zenu, Ahadi yangu leo imepata ufumbuzi wa kudumu baada ya kuwatengenezea wananchi mfumo wa ki-elektoniki wa malalamiko ambao nimeuzindua rasmi,” amesema Rais Dkt.Mwinyi hivi karibuni.

Zifuatazo ni namba za taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na zile za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizounganishwa kupitia mfumo wa Sema na Rais Mwinyi;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Hello Sir/Madam.
    I'm a graduate from the State University of Zanzibar who took a degree in Information technology application and management. I'm looking for an opportunity to work at at any government institution, can I get a help on how and where do I start the application please?

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news