Ni Kinana baada ya Mangula kung'atuka

*Akiwa ni msomi makini wa uchumi na mwanajeshi wa kusomea, Kinana anatajwa kuwa ni mtu mnyenyekevu aliyekalia hazina kubwa ya ujuzi na historia ya chama na serikali zake zote

NA GODFREY NNKO

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi-CCM (NEC) imempitisha na kumpendekeza Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, ndugu Abdulrahman Kinana kuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara).
Ni baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, ndugu Philip Mangula kung’atuka katika nafasi hiyo aliyehudumu kwa muda.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo leo Machi 31, 2022 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa NEC uliofanyika chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Akiwa ni msomi makini wa uchumi na mwanajeshi wa kusomea, Kinana anatajwa kuwa ni mtu mnyenyekevu aliyekalia hazina kubwa ya ujuzi na historia ya chama na serikali zake zote.

Pia Kinana ni hodari wa diplomasia, mwenye uwezo wa kubakia katika uhusiano na mahasimu wake kisiasa bila kuathiri maslahi ya chama muda wowote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news