Orodha mpya ya majina ya balozi na viongozi mbalimbali walioteuliwa leo na Rais Samia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo;
Amemteua Bwana Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bwana Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Mwita Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Pia amewateua Bwana Humphrey Hezron Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Ibara ya 67(2) (g) ikisomwa pamoja na Ibara ya 71(1)(a).

Mheshimiwa Rais Samia amewateua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority) na Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

Aidha, amemteua Bwana Peter Rudolph Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (Tanzania Telecommunication Corporation Limited – TTCL) na Bwana Nehemia Kyando Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation). 

Bwana Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Bwana Mchechu aliwahi kutumikia Shirika la Nyumba (NHC) huko nyuma kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani, atapangiwa kazi nyingine.

Bw. Kindamba na Balozi Mteule Polepole wataapishwa tarehe 15 Machi, 2022 saa 04:00 asubuhi viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news