Profesa Jay atawala Tamasha la Serengeti

*Mamia ya Watanzania wacheza nyimbo zake na kumuombea

NA JOHN MAPEPELE

WASHEREHESHAJI wakongwe nchini B12 na Samio love wote kutoka kituo cha Redio cha EFM na Televisheni ya ETV wamewaongoza wamia ya watu waliohudhuria Machi 12, 2022 Tamasha la Muziki la Serengeti kucheza nyimbo za Mwanamuziki nguli nchini Profesa Jay ikiwa ni ishara ya kumuenzi na kumuombea kwa mwenyezi Mungu ampe heri kwenye maradhi yanayomkabili hivi sasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemwelezea Profesa Jay kama Mwanamuzi ambaye ametoa mchango mkubwa kwenye muziki wa kizazi kipya.

Wakati vikipigwa vibao kadhaa vya Profesa Jay umati wote uliimba kwa hisia kali nyimbo hizo utadhani ni kwaya iliyofundishwa na mwalimu mmoja.

Kwa hakika hata kama hajashiriki tamasha la Serengeti moja kwa moja kwenye uwanja wa Chinangali, historia imeandikwa kwa kuteka mioyo ya watu.

Awali, siku moja kabla ya tamasha la Serengeti wakati wasanii walipotembelea Ofisi ya Utamaduni, Sanaa na Michezo eneo la Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi aliishukuru Serikali kwa uamuzi wa kugharimia matibabu na kuwasihi wasanii wito kuendelea kumwombea.

Mwenyezi Mungu ampe wepesi apone mapema na kurejea katika majukumu yake ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news