NA GODFREY NNKO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Yusuf Juma Mwenda kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 1,2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza leo Machi 1, 2022.
Aidha,kabla ya uteuzi huo Yusuf Juma Mwenda alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kutengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya upotevu wa fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.
Tags
Habari