NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MKURUGENZI wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN Women) Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Maxime Houinato akiwa amefuatana na ujumbe wake wamefika Ikulu jijini Zanzibar kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Maxime Houinato, alipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yaliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dr. Maxime Houinato, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yaliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Kiongozi huyo ametumia fursa hiyo kumpongeza kwa jinsi anavyozingatia suala zima la usawa wa kijinsia katika uteuzi wake wa viongozi.
Mkurugenzi huyo pia amehidi kwamba UN WOMEN itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mikakati yake ya kuwaunga mkono wanawake katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dk.Maxime Houinato baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kujitambulisha. na (kushoto kwa Rais) Mwakilishi wa UN Women Bi. Hodan Addou.
Nae Rais Dkt.Mwinyi kwa upande wake alimuelezea kiongozi huyo mikakati mbalimbali iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakaikisha wanawake na watoto wanapata haki zao za msingi.
Aidha, alieleza hatua zilizowekwa na serikali anayoiongoza katika kuwawezesha wanawake.