Rais Dkt.Mwinyi awaapisha viongozi mbalimbali

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri pamoja na Makamishna.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Jamal Kassim Ali kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar,hafla hiyo ya kuapishwa ilimefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Machi 10,2022 katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakuu wa Kitaifa, Mawaziri, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa pamoja na watendaji wengine wa Serikali.

Miongoni mwa viongozi walioapishwa ni Jamal Kassim Ali ambaye anakuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais–Ikulu, Dkt. Saada Mkuya Salum anayekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Harusi Said Suleiman anayekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan Juma, Dkt. Khalid Salum Mohamed anayekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassim Ali, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhamed Mussa, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis, Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Shaib Hassan Kaduara.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed kuwa Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Nassor Ahmed Mazrui kuwa Waziri wa Afya Zanzibar,hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Riziki Pembe Juma kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Simai Mohammed Said kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Suleiman Masoud Makame kuwa Waziri wa Uchumi wa Buluu, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaapisha Manaibu Waziri akiwemo Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Juma Makungu Juma, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Hassan Khamis Hafidh, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Ali Suleiman Ameir (Mrembo), Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Nadir Abdullatif Yussuf Alwardy, Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Abdulgullam Hussein, Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anna Athanas Paul pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Maji, Nishati na Madini ambaye anakuwa Shaaban Ali Othman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Harusi Said Suleiman kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Hamza Hassan Juma kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Rahma Kassim Ali kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Lela Mohammed Mussa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Shamata Shaame Khamis kuwa Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji, Maliasili na Kilimo Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Shaib Hassan Kaduara kuwa Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Juma Makungu Juma kuwa Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Hassan Khamis Hafidh kuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Ali Suleiman Ameir (Mrembo) kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar,hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Pia, Rais Dk. Mwinyi amemuapisha Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Balozi Mohamemd Mwinyi Mzale pamoja na kumuapisha Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar Yussuf Juma Mwenda.

Baadhi ya viongozi walioapishwa walifanya mahojiano na waandishi wa habari na kueleza jinsi walivyofarijika na uteuzi walioupata na kuahidi kwamba watamsaidia na kumuunga mkono Rais Dkt. Mwinyi katika kuhakikisha anatekeleza vyema kiu yake ya kuiletea maendeleo endelevu Zanzibar pamoja na watu wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news