NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika na kujenga mazingira mazuri ili Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) iendelee kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkufunzi Kikundi cha Watu Wenye Ulemavu Zanzibarm, Bi. Njuma Ali,wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki jijini Zanzibar leo Machi 5, 2022 (kushoto kwa Rais) ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB, Bw.Edmund Mndolwa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyamesema hayo leo wakati akizindua Kongamano la Wanawake kuhusu Nafasi ya Mwanamke katika Kukuza Uchumi wa Buluu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, iliyopo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ambapo Mama Mariam Mwinyi nae alihudhuria.
Katika maelezo yake Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuunganisha benki ndogo ndogo zilizokuwepo awali kwa lengo la kuunda Benki ya TCB umelenga kuyanufaisha makundi mbalimbali ya wafanyabiashara, wawekezaji, wajasiriamali na wananchi kwa jumla.
Hivyo Rais Dkt.Mwinyi amehimiza benki hiyo kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili malengo ya Serikali ya kuianzisha na kuiimarisha benki hiyo yaweze kufikiwa kwa maslahi mapana ya nchi.
Ameitaka benki hiyo kuongeza juhudi za kuwa wabunifu ili taasisi hiyo isiyumbe, iendelee kuwa imara na yenye uwezo na nyenzo za kuhimili ushindani mkubwa uliopo ndani na nje ya nchi katika sekta ya huduma ya fedha. “Kuweni mstari wa mbele katika mageuzi ya kiuchumi yaliyopangwa na Serikali zetu katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Dkt.Mwinyi.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na taasisi za fedha pamoja na wawekezaji wa ndani na nje katika juhudi za kuendeleza uchumi wa buluu na kuhimiza kuzitumia kikamilifu fursa zinazotolewa na benki za hapa nchini.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amezihimiza benki za hapa nchini kuendelea kushirikiana na wajasiriamali kwa kuwapatia mikopo yenye unafuu wa riba na kuendela kuzisogeza huduma za fedha karibu na maeneo yao ya kazi,kuwapatia mafunzo pamoja na kuwapatia masoko.
Ameeleza kuwa, uamuzi wa benki hiyo wa kutoa elimu na kuhamasisha wanawake kushiriki katika kutekeleza mipango inayohusu uchumi wa buluu ni muhimu ikizingatiwa kwamba uchumi wa buluu umejumuisha sekta kadhaa zikiwemo uvuvi, utalii, usafiri wa bahari, ujenzi wa bandari za kisasa, kilimo cha mwani, uchimbaji wa mafuta na gesi na matumizi mengineyo ya rasiliamali za bahari kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira. Amesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi za kina mama katika kuendeleza zao la mwani ambalo ni sehemu ya uchumi wa buluu, hivyo kupitia kongamano hilo anaamini kwamba mipango na mikakati ya kuliendeleza zao hilo kwa matumizi ya mbegu bora pamoja na mbinu za kuliongezea thamani na utafutaji wa masoko itajadiliwa.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea na jitihada za kuwapatia mitaji, vifaa na masoko wazalishaji wa mwani wa Unguja na Pemba kwani imeweka mkazo maalum wa kuyapatia mikopo makundi mbali mbali ya wanawake wanaojishughulisha na uzalishaji mwani na shughuli nyengine za biashara.
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuvutiwa kwake na uamuzi na utaratibu wa Benki ya Biashara Tanzania wa kuweka mkakati maalum wa kuandaa na kuendesha makongamano malaum ya wanawake kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya wanawake kwa lengo la kustawisha ustawi wa wanawake nchini.
Nae Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui alitoa pongezi zake kwa Rais Dkt.Mwinyi kwa juhudi zake za kuwakomboa wananchi kiuchumi na kusisitiza kwamba hatua zake hizo zitaendelea kuungwa mkono kwani ana nia njema ya kuwasaidia wananchi wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Dkt. Edmund Mndolwa alieleza kwamba licha ya changamoto kadhaa inazozipata benki hiyo, lakini hata hivyo imeweza kupata mafanikio makubwa na kueleza matumaini yake kwamba benki hiyo ndani ya miaka mitano itakuwa ni benki ya mfano hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi alieleza matumaini yake makubwa ya maendeleo yatakayofikiwa na Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt.Mwinyi.
Amesema kuwa Benki hiyo ya Biashara (TCB) ni Benki kongwe ambayo ina miaka 97 tokea kuanzishwa kwake na ambayo inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 83, Shirika la Posta Tanzania asilimia 8, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar asilimia 3, Posta na Simu asilimia 3 na Mfuko wa Hifadhi wa Jamii kwa watumishi wa Umma asilimia 2.
Katika hafla hiyo Rais Dkt.Mwinyi alitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wa benki hiyo vikiwemo vikundi vya wajasiriamali, Taasisi ya Maisha Bora ‘Zanzibar Maisha Bora Foundation’ pamoja na kukabidhiwa kadi yake ya uwanachama wa benki hiyo.
Mapema Rais Dkt.Mwinyi alipata fursa ya kukagua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali waliokuwepo hotelini hapo katika hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB, Bw.Edmund Mndolwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bw, Sabasaba Moshingi na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Bw.Rashid Simai Msaraka alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika ukumbi wa hoteli hiyo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB.Bw.Edmund Mndolwa, wakimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha Zaidat Product cha Chukwani Zanzibar.Bi. Tatu Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania.(TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB.Bw.Edmund Mndolwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB )Bw.Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar, akieleza huduma zinazotolewa na Benki hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB )Bw.Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) KATIKA ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar, kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmin RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kulifungua Kongamano hilo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo 5-3-2022, lililowashirikia Wanawake Wajasiriamali wa Vikundi mbalimbali vya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo 5-3-2022, lililowashirikia Wanawake Wajasiriamali wa Vikundi mbalimbali vya Zanzibar
Wakurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano wa Wajasiriamali Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na (TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo 5-3-2022 na kuwashirikia Wajasiriamali Wanawake wa Zanzibar.
Wafanyakazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano wa Wajasiriamali Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na (TCB) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki jijini Zanzibar leo na kuwashirikia wajasiriamali wanawake wa Zanzibar.