Rais Samia aagiza mabadiliko yafanyike kwa taasisi hizi

*Ataka MSD ifanyiwe mabadiliko ngazi zote

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kufanywa mabadiliko katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwenye ngazi zote za utendaji kazi.
Ametoa agizo hilo leo Machi 30,2022 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). (Picha na Ikulu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP Salum Hamduni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.

Mheshimiwa Rais Samia amesema, mabadiliko hayo ni kutokana na bohari hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika kuhudumia soko la nchi za Jumuiya ya Maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC).

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameagiza taasisi za Serikali zinazokopa mikopo chechefu kutoka mifuko ya hifadhi za jami zirejeshe mikopo hiyo na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika mifuko hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. 

Pia ameagiza kufanyike ukaguzi na tathimini ya mashirika ya umma na kuyafuta ambayo hayana tija kwa Taifa, kwani mpaka sasa mashirika 38 yanaendeshwa bila Bodi ya Wakurugenzi.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia ameitaka Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kuzisimamia halmashauri ipasavyo na kuwachukulia hatua watumishi wenye matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameipongeza TAKUKURU kwa kuweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kuitaka taasisi hiyo kujielekeza zaidi katika kuzuia kuliko kupambana na rushwa.

Aidha, amempongeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kuweza kupunguza kiwnago cha hati chafu na kuweza kudhibiti usimamizi wa rasilimali za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news