Rais Samia amteua Nehemia Mchechu kuwa bosi wa NHC, alisimamishwa kazi mwaka 2017

>Mchechu aliteuliwa kuliongoza shirika hilo Machi 1, 2010
 
NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua Bw.Nehemia Kyando Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation-NHC).

Uteuzi ho ambao umeanza mara moja umefanywa leo Machi 14, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Bi.Zuhura Yunus.
Mchechu ambaye aliwahi kuliongoza shirika hilo kwa miaka kadhaa huko nyuma na kutajwa kuwa miongoni mwa viongozi ambao waliliwezesha kufanya vizuri kupitia miradi mbalimbali alisimamishwa kazi Desemba 16, 2017.

Taarifa ya kusimamishwa kazi kiongozi huyo ilitolewa tarehe ambayo ilikuwa ni siku ya Jumamosi na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akieleza uamuzi huo ulitolewa na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Mchechu aliteuliwa kuliongoza shirika hilo Machi 1, 2010. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA.

Aidha, taarifa ya Dkt.Abbasi siku hiyo ilieleza kuwa,, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Mheshimiwa Lukuvi alichukua uamuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu F. 35 (1) cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.

Mbali na Mchechu, Lukuvi wakati huo aliitaka bodi ya shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Huduma za Mikoa na Utawala, Raymond Mndolwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news