Serikali ya Zanzibar yaonesha upendo wa kipekee kwa watalii raia wa Ukraine

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WATALII zaidi ya 900 raia wa Ukraine wamekwama Zanzibar baada ya muda wao wa kukaa visiwani humo kuisha huku wakikosa fedha za kuendelea kulipa hoteli.

Hata hivyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeingilia kati suala hilo na kuangalia njia bora ya kuwasaidia watalii hao.
Akitolea ufafanuzi suala hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari Februari 28, 2022 Ikulu jijini Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inafanya mpango kuhakikisha raia hao wanaendelea kuwa salama.

"Taarifa nilizonazo kuna watalii wa Ukraine kama 900 hivi wapo Zanzibar na hawawezi kurudi kwao, wameomba msaada ili Serikali iwasaidie hawawezi kuendelea kukaa hotelini kwa sababu hawana fedha, lakini tumeanza mazungumzo wale wenye hoteli pamoja na Serikali tunazungumza kuona kwa jinsi gani tutawasaidia.

"Tunaangalia namna ya kuwasaidia mpaka Serikali yao itakapopata uwezo wa kuleta msaada, kwa hiyo kuna makubaliano ambayo yameanza kuonekana na hoteli kuwapa msaada bila ya kuwachaji,lakini na Serikali kuwaangalia wale wenye hoteli kwa upande wa kodi,kwa hiyo tunazungumza, ukweli ni kwamba tunaona umuhimu wa kutoa msaada," amesema Rais Dkt. Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news