Serikali yadhamiria kuimarisha kilimo, masoko ya viungo vya chakula na vikolezo

NA MWANDISHI MAALUM-TARI

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na Wakala wa Mbegu Tanzania(ASA) wametakiwa kuhakikisha wanafanya utafiti wa mbegu na kuzalisha mbegu kwa wingi za mazao ya viungo na vikolezo ili kuinuia tasnia ya mboga mboga na matunda nchini.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Anthony Mavunde wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kujionea mashamba ya uzalishaji mbegu ya ngano,maharage na mazao ya mboga mboga na bustani yaliyopo maeneo ya Ngaramtoni na Tengeru pamoja na Kituo cha Utafiti wa Kilimo wa mazao ya mboga mboga na bustani-TARI Tengeru.
"Serikali imedhamiria kuweka nguvu katika kuimarisha kilimo cha mboga mboga na bustani ili kitoe mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu,kutoka katika mauzo ya dola milioni 750 kwa mwaka kufikia dola bilioni 2 ifikapo mwaka 2030,"amesema Mheshimiwa Mavunde.
Amesema kuwa, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kwa kuitangaza Kimataifa hali itakayopelekea kupatikana kwa masoko ya uhakika ya mazao yetu ya mboga mboga na matunda.

"Lazima uzalishaji wa miche bora ya matunda na mbegu bora za mboga mboga uongezeke kutoka uzalishaji wa sasa ili tuweze kufikia malengo haya ya soko la Kimataifa,"amesema.
Ameongeza kuwa, "TARI hakikisheni mnafanya utafiti wa kutosha katika eneo la viungo na vikolezo,eneo hili lina fursa nyingi sana, lakini bado halijafanyiwa utafiti wa kutosha ili tuweze kuzalisha aina mbalimbali za mbegu bora za viungo kwa ajili ya soko la Kimataifa,Serikali inatambua umuhimu wa utafiti ndio maana bajeti katika eneo hili imeongezeka kufikia bilioni 11.7 kufikia 2022,"amesema.

Pia kwa ASA amesema, "hakikisheni mnaongeza uzalishaji wa miche mingi zaidi na mbegu bora za kuwezesha wakulima kulifikia soko la Kimataifa,shirikisheni sekta binafsi na hasa Chama cha Wadau wa Viungo na Vikolezo ili kutambua mahitaji ya soko na aina gani za mbegu zizalishwe kwa wingi kwa kwa wakati huu,”amesema Mavunde.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watendaji wa ASA na TARI wameahidi kufanyia kazi maelekezo hayo kwa uharaka ili kukuza tasnia ya mboga mboga na matunda na hasa katika eneo hilo la viungo na vikolezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news