Serikali yajiimarisha ukaguzi wa dawa na bidhaa za afya nchini, yatoa angalizo kwa waganga wakuu

NA MWANDISHI MAALUM, OR- TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Dkt. Grace Magembe amesema kuanzia sasa ukaguzi wa bidhaa za afya kitakuwa ni moja ya kiashiria cha ufanisi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri.
Ameyasema hayo Machi 3,2022 alipofanya ukaguzi wa ubora wa utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri ya Gairo na Mvomero mkoani Morogoro ulioambatana na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ya afya inayoendelea kutekelezwa.

Dkt. Grace amesema kuwa, kutofanyika  kwa ukaguzi wa dawa na bidhaa za afya kunaweza kuchangia  upotevu na matumizi  mabaya ya bidhaa za afya ikiwemo dawa, vitendanishi na vifaa tiba.
Amesema, kazi ya ukaguzi wa bidhaa za tiba sasa lazima ifanyike kwa ushirikiano kati ya Idara ya Afya   na Wakuu wa Idara  nyingine wakiwemo wakaguzi wa ndani.

Amemuagiza  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na  Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  kufanya ukaguzi wa bidhaa za afya  kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mvomero  na kuwasilisha taarifa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI  ndani ya siku saba kufuatia  ukaguzi wa awali kuonesha kuna bidhaa ambazo  takwimu zake hazikuwa na uhalisia 
Aidha, amemuelekeza Mkurugenzi huyo kuanza mara moja ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) na kumtaka Mhandisi wa Halmashauri kutoa utaalam wa kiufundi wa namna bora ya kuweka mifereji ya kuondoa maji yanayotuama katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news