NA MWANDISHI MAALUM
SERIKALI imesema imepiga hatua kubwa katika
kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini kwa kutelekeza
programu mbalimbali za utoaji elimu na huduma kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Balozi Dk. Pindi Chana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake kuhusu mafanikio ya Ofisi yake kwa Kipindi cha mwaka mmoa wa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika tarehe 9 Machi, 2022 katika Ofisi zake zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.(Picha na OWM).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Balozi Dkt. Pindi Chana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akitoa taarifa ya mafanikio ya Ofisi yake katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Balozi Dk. Pindi Chana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake kuhusu mafanikio ya Ofisi yake kwa Kipindi cha mwaka mmoa wa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika tarehe 9 Machi, 2022 katika Ofisi zake zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Pindi amesema miongoni mwa hatua kubwa zilizopigwa na serikali ni pamoja na kudhibiti vifo vitokanavyo na UKIMWI ambapo vimepungua kwa asilimia 50 kutoka 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2021.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja mafanikio ya Serikali yaliyoshuhudiwa katika eneo hili ni kupungua kwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU katika jamii ikiwemo maambukizi mapya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kushuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2021,” amesema Pindi.
Akibainisha mafanikio mengine katika mapambano dhidi ya UKIMWI alisema kwamba ni kushuka kwa kiwango cha unyanyapaa katika jamii kutoka asilimia 28 mwaka 2013 hadi asilimia 5.5 mwaka 2021, na Nchi kuwa katika hatua nzuri za kufikia malengo ya Kidunia ya Tisini Tatu (90-90-90) mwaka 2020 na Tisini na Tano Tatu (95-95-95) mwaka 2025.
“WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi ni asilimia 83, WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi na wapo kwenye matibabu ni asilimia 98 na WAVIU waliopo kwenye matibabu na wamefubaza VVU ni asilimia 92,”ameeleza Waziri Pindi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Mhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Saudeni Ananic alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Awamu ya pili wa jengo la Ofisi yake lililopo Mji wa Serikali Mtumba mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Kuhusu mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, Pindi alisema Kliniki sita za tiba ya Methadone zimeanzishwa katika mikoa ya Songwe, Arusha na zingine nne jijini Dar es Salaam hivyo kufanya kliniki hizo kufikia 15 nchi nzima zinazohudumia zaidi ya waathirika 10,600 wa dawa za Kulevya kila siku.
“Serikali imekuwa ikisimamia upatikanaji wa uhakika wa dawa ya Methadone kwa ajili ya tiba ya waraibu wa Heroin kwa kusimamia uagizaji, usambazaji na udhibiti wake na ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi vijana 200 wanaopatiwa matibabu kwenye kliniki za Methadone wamejumuishwa katika Programu ya Kukuza Ujuzi kupitia Vyuo vya VETA ili kuwajengea ujuzi wa kufanya kazi za kiuchumi,”amefafanua Pindi.
Naibu Katibu Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Kaspar Mmuya (kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Batholomeo Jungu (kulia) wakifuatilia mkutano huo.
Aidha, alieleza kwamba serikali imekuwa ikitoa elimu kwa njia
mbalimbali ambapo vilabu vya kupinga dawa za kulevya vimeanzishwa
shuleni na walimu 66 wamepatiwa elimu ili kuwawezesha kusimamia klabu
hizo, vyuoni na elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya ambapo
inakadiliwa zaidi ya wananchi millioni 10 wamefikiwa na elimu hiyo.
“Serikali
imeendelea kuhakikisha inadhibiti matumizi na usambazaji wa dawa za
kulevya kwa lengo la kuwanusuru wananchi wake kuathirika na dawa hizi
kwahiyo hatua hii ya Serikali imesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia wimbi
la vijana kuingia kwenye matumizi na biashara ya dawa hizo,” amesema. Mkuu wa kitengo cha Mawasilino Ofisi ya Waziri Mkuu, Augustino Tendwa akiongoza mkutano wa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ofisi hiyo katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita jijini Dodoma. Naibu Katibu Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Kaspar Mmuya akifafanua jambo kwa wandishi wa habari kuhusu masuala ya uratibu wa shughuli za Serikali wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Majengo ya ofisi hiyo kwa Awamu ya Pili.
Pia akitaja mafanikio mengine ya Serikali ya Awamu ya Sita alifafanua
kuwa ni pamoja na Uzinduzi wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali ambao
unaendelea na ukitarajiwa kukamilika mwaka 2022/23.
“Ujenzi wa
miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara zenye urefu wa KM 51.2 katika
mji huo zinajengwa kwa kiwango cha lami. Katika mwaka 2021/22 jumla ya
Sh bilioni 300 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi na
Miundombinu,”alibainisha.