Serikali yatenga Bilioni 1/- za mafunzo ya waongoza watalii wanawake nchini

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO -19 imetenga shilingi bilioni 1.01 kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake takribani 1060 nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya waongoza Watalii wanawake 89 yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA), Prof. Jafari Kideghesho akitoa neno la utangulizi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

“Mafunzo haya ni mahususi kwa wanawake kama jitihada za makusudi kabisa za Serikali kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa za kuchangia katika maendeleo ya nchi kupitia utalii na kunufaika kupitia sekta hiyo,"amefafanua Mhe. Masanja.

Amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa kuitangaza vyema Tanzania ndani na nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt. Consolatha Kapinga akielezea namna Serikali ilivyojipanga kuwawezesha wanawake hasa kuwajengea uwezo waongoza watalii, wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya waongoza watalii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsilikiza Kiongozi Mkuu wa Waongoza Watalii Wanawake Tanzania,Maggie Dankan Simbeye (kulia) akifafanua kuhusu hema linalotumika kiutualii alipowasili kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

“Natambua mmekuwa mabalozi muhimu mnaotegemewa kuiuza nchi yetu hivyo sifa ya kwanza mnayotakiwa kuwa nayo ni uzalendo. Wageni mnaowapokea wana sifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa hivyo wakati mnatekeleza majukumu yenu mnapaswa kuwa na uelewa mpana wa shughuli za utalii na pia muwe na maadili, weledi na uadilifu,”amesema Mhe. Masanja.

Aidha, amewaasa waongoza watalii hao kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watalii wanapowasili nchini ili kujenga taswira nzuri ya Tanzania na kumfanya mtalii aweze kurudi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news