NA MWANDISHI DIRAMAKINI
NI wazi kuwa, Klabu ya Simba imedhamiria kusonga mbele katika michuano inayowakabili ikiwemo ya Kitaifa na Kimataifa ambapo kwa sasa wamejichimbia huku wakipiga zoezi kali.Wimbo wao ukiwa kila watakaye kutana naye ni halali yao.
Ni katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo, leo Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na ushindi na 2-1 kwenye mchezo katika mechi
ya kirafiki dhidi ya Cambiasso kwenye dimba la Mo Simba Arena huko Bunju jijini Dar es Salaam.
Simon Msuva ndiye aliyeipatia Cambiasso bao huku upande wa Simba SC yakifungwa na Erasto Nyoni na Clatous Chama.