Taasisi wezeshi zapongezwa kwa kutoa huduma bora kwa wawekezaji Zegereni

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TAASISI wezeshi wilayani Kibaha zimepongezwa kwa kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa viwanda kwenye eneo la Zegereni ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya viwanda.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea eneo hilo ili kujua changamoto zilizopo kwenye eneo hilo ili zipatiwe ufumbuzi, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi.Sara Msafiri alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko juu ya huduma zilizokuwa na watumishi wa idara mbalimbali.
Akizungumzia upande wa miundombinu yote inayohitajika ili kuwaondolea changamoto wawekezaji wa viwanda amesema kuwa, miundombinu hiyo ni pamoja na ile ya umeme ambapo kutakuwa na umeme wa viwanda pekee kwenye eneo hilo kwani uliopo hauna nguvu ya kutosha.

Aidha, alisema kuwa miundombinu mingine ni bomba maalumu la maji na barabara kiwango cha lami ambapo kwa sasa imewekwa sehemu ndogo.
Naye ofisa rasilimali watu wa kiwanda cha mabomba ya chuma Jafra Investment Supplies Company LTD, Metsedeck Piason alisema kuwa kiwanda hicho kinazalisha tani 40 kwa siku.
Kwa upande wake, Prosper Ernest wa kiwanda cha BNBM Building Materials kinachojihusisha na utengenezaji wa marumaru alisema kuwa, changamoto kubwa ni bidhaa za aina hiyo kuingizwa nchini na kuwafanya soko lao kuwa dogo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news