NA MWANDISHI DIRAMAKINI
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Novatus Dismas Miroshi, wa Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Israel dakika ya 10 na washambuliaji, Nahodha Mbwana Ally Samatta wa Royal Antwerp ya Ubelgiji dakika ya 63 na George Mpole Mwaigomole wa Geita Gold ya nyumbani dakika ya 90 ndiyo waliowapa raha Watanzania.
Aidha, bao pekee la CAR limefungwa na mshambuliaji wa Gasogi United ya Rwanda, Christian-Theodor Yawanendji-Malipangou kwa penalti dakika ya 66.
Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen itacheza mechi mbili zaidi katika kalenda ya FIFA.
Mechi nyingine itakuwa dhidi ya Botawana Jumamosi na dhidi ya Sudan Machi 29, zote katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.