Tanzania kufaidika zaidi kwa utunzaji wa rasilimali maji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi (Mb) amesema Tanzania inaendelea kunufaika pamoja na wananchi wake kwa kujenga uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali, zikiwemo nchi jirani zinazoizunguka.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Maryprisca Mahundi (Mb) akiongoza Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la mto Songwe uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi ambapo masuala ya rasilimali za maji yanayozihusu nchi za Tanzania na Malawi yamefanyiwa kazi kwa ushirikiano na wataalamu wa pande zote mbili za nchi hizo. Kushoto ni Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Malawi Mhe. Abida Sidik Mia (Mb).

Mhe. Mahundi amesema hayo wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Amesema, kupitia Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe kazi inafanyika kwa ushirikiano kuondosha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Tanzania na Malawi kupitia wataalamu wa rasilimali za maji, ikiwemo ujenzi wa mabwawa katika bonde hilo ambayo itakuwa suluhu ya mafuriko yanayoharibu mali mbalimbali ikiwamo mazao kwa kujenga bwawa la Songwe Chini, na mazingira.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) akipitia makabrasha kuhusu Mkutano Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la mto Songwe Jijini Lilongwe. Wizara ya Ardhi ni moja ya wizara muhimu katika kufanikisha kazi mbalimbali za maendeleo ya wananchi katika bonde hilo.

Aidha, kuwezesha kilimo cha umwagiliaji zaidi ya hekta 6,000 na kupata nishati ya uhakika ya umeme kwa nchi mbili kugawana megawati zipatazo 180.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi (Mb) pamoja na Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Malawi Mhe. Abida Sidik Mia (Mb) wakisaini makubaliano ya kuendesha vikao vya Mawaziri vinavyohusu Kamisheni ya Bonde la mto Songwe, tukio limefanyika Lilongwe nchini Malawi.

Mhe. Mahundi amesema hayo ni mafanikio ya mahusiano yaliyojengwa na viongozi wa nchi mbili katika kuhakikisha wananchi wanafanya kazi kwa maendeleo ya nchi zao. Amesema kazi hiyo ni matunda ya viongozi Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mhe. Lazarus Chakwera , Rais wa Malawi.

Pamoja na hatua hiyo, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili kuhakikisha huduma ya maji na miradi ya maji inakuwa endelevu na kutosheleza mahitaji ya jamii kwa sasa na vizazi vijavyo.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la mto Songwe uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi. Katikati ni Dkt. George Lugomela, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Tanzania.

Kamisheni ya Bonde la mto Songwe inaundwa kwa Pamoja na nchi za Malawi na Tanzania, ambapo katika kikao hicho Mawaziri wamekubaliana na kusaini Kanuni za uendeshaji wa vikao vya Mawaziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news