TARI Naliendele yaeleza Mtwara walivyo na uwanda mpana kustawisha mazao mengine bila kuathiri zao la korosho

*Tafiti za kilimo cha mboga na matunda (hotculture) zaonesha matokeo bora

NA MWANDISHI MAALUM

MKURUGENZI wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, TARI Naliendele Dkt.Fortunus Kapinga amesema kuwa tekolojia ya Mtwara inaruhusu wakulima wa Mtwara kulima mazao mengi yakiwemo mazao ya bustani, jamii ya kunde na nafaka bila kuathiri kilimo cha zao la korosho.

Hivyo wanaweza kujiongezea kipato kutoka kwenye mazao hayo badala ya kutegemea zao la korosho peke yake.
Dkt.Kapinga alisema kuwa mahitaji ya kiikolojia ni mojawapo ya sababu zinazowafanya washauri zao fulani lipandwe wapi, lini na vipi.

Dkt.Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi kutoa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo cha Kilimo Borigaram - Kigamboni walioko kituoni hapo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Field Practical) katika taasisi hiyo.
Wakizungumzia tafiti za kilimo cha mboga na matunda (hotculture) wanafunzi hao wamesema wameshangaa kuona migomba ikistawi na kuzaa kwa wingi na kudai kuwa wakazi wa Mtwara wanaweza kutengeneza kipato kikubwa wakati wakisubiri mavuno ya mazao mengine kama vile Korosho na Ufuta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news