TARURA yaanza ujenzi wa daraja la Mwasanga

NA MWANDISHI MAALUM-TARURA

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza ujenzi wa daraja la Mwasanga linalounganisha Kata za Mwasanga, Tembela na Mwakibete jijini Mbeya.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Wilson Charles alisema ujenzi wa daraja hilo utakaogharimu Shilingi Bilioni 1.4 unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi.

“Fedha kwa ajili ya mradi huu tulishaletewa na Serikali na kilichobaki sasa ni ujenzi ambao tayari umeshaanza kama mnavyoona, tutasimamia ili kuhakikisha unakamilika ndani ya muda uliopangwa,” alisema Mhandisi Charles.
Diwani Kata ya Tembela, Frank Mwasyoke ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Kata ya Tembela, Mwasanga na Mbeya vijijini kwa kuimarisha shughuli za kiuchumi na za kijamii.
Naye Mkazi wa Kata ya Tembela, Bw. Joseph Mpole ameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa daraja hilo ambalo walikuwa wanapata shida kuvuka baada ya kuvunjika lakini kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutawasaidia katika kusafirisha mazao yao na kuzifikia huduma za kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news