NA MWANDISHI MAALUM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuwasisitiza wataalamu mbalimbali kuwa uandaaji wa viwango ni shirikishi, lengo ni kutoa uhakikisho wa ubora, usalama, kuaminika na ufanisi.
Baadhi ya watumishi wa TBS na wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika Makao Makuu ya TBS jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesema Machi 21, 2022 jijini Dar es Salaam katika mkutano baina ya shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari ambapo imeelezwa kuwa wanahabari wakatapokuwa na uelewa wa masuala mbalimbali yahusuyo TBS itasaidia kurahisisha kufikisha elimu kwa jamii namna bora ya masuala ya viwango.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bi.Viola Masako akifungua mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika makao makuu ya TBS jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Viola Masako amesema kuifahamu elimu ya viwango ina faida mbalimbali ikiwemo kuipa Serikali urahisi wa kuunga sheria zinazohusiana na masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango,Meneja wa Viwango, Yona Afrika amefafanua kuwa kiwango kinapokuwa cha kitaifa utekelezaji wake ni mwananchi yeyote huku akizitaja faida za viwango kuwa ni pamoja na urahisishaji wa biashara.
Kaimu Mkurugenzi wa Uandaaji Viwango (TBS), Mhandisi Yona Afrika akizungumza katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
"Faida nyingine za viwango hulinda afya na usalama wa walaji au watumiaji wa bidhaa mbalimbali, lakini pia huondoa mkanganyiko kuhusiana na bidhaa,"amesema Mhandisi Yona.
Kwa upande wake Meneja wa Upimaji TBS, Joseph Makene akiwasilisha mada kuhusu huduma zitolewazo na kurugenzi ya upimaji na ugezi amesema, vifaa vinavyotumika katika maabara zilizopo katika shirika hilo ni vya kisasa na vinatumia teknolojia ya kisasa.
Afisa Habari na Mawasiliano TBS, Bi.Neema Mtemvu akizungumza katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika makao makuu ya TBS jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa TBS pia hutoa huduma ya kuratibu na kuthibitisha ubora wa biadhaa kwa kutumia viwango vya kampuni,vya kigeni au vya kimataifa vilivyothibitishwa na kamati maalum hususani pale ambapo hakujawa na kiwango cha kimataifa cha bidhaa husika.