TGNP yashiriki Kongamano la Kitaifa la Wanawake jijini Arusha

NA KADAMA MALUNDE

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeshiriki Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha kwa lengo la kuwakutanisha wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili wanawake na ustawi wao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.(Picha zote na Malunde 1 blog).

Kongamano hilo limeongozwa na kauli mbiu ‘Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa’.

Akifungua Kongamano hilo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kwa kuwezesha wanawake kufikia kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (kulia) akifuatilia hotuba ya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake.

Mpanju amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia kumefanyika mapinduzi makubwa na hatua kubwa imepigwa katika kujenga kizazi cha haki na usawa huku wanawake wakichaguliwa na kuteuliwa kuongoza Idara nyeti katika taifa.

“Wanawake ni nguzo ya maendeleo duniani. Ndani ya mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia tumepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja, tuna Rais Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke, Katibu Mkuu wa Bunge mwanamke, tuna Mawaziri wanawake 9 katika Wizara nyeti wanafanya kazi vizuri na maendeleo tunayaona, mambo yanakwenda vizuri,”amesema Mpanju.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (wa pili kushoto) akiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake.
Mpanju amewataka wadau na wananchi kwa ujumla kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike akiongeza kuwa ni vyema jamii ikapambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

Amesema, jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news