NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KWA mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Mkoa wa Ruvuma,Mtwara, Lindi, Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Geita, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mchambuzi: Godfrey Kazinja kutoka TMA.
Aidha, Mkoa wa Mara unatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Huku mikoa ya Dodoma na Singida ikitarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Wakati huo huo, TMA kupitia utabiri wa leo Machi 2, 2022 kuanzia saa 9:00 usiku wa leo inaeleza kuwa, Mkoa wa Simiyu, visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Upepo wa Pwani
Kwa mujibu wa TMA, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kutoka Kaskazini Magharibi kwa Pwani ya Kusini na kuvuma kwa kasi ya kilomita 40 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini.
Aidha, hali ya bahari inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi hadi makubwa huku matarajio kwa siku ya Ijumaa ya tarehe 04/03/2022 kutakuwa na mabadiliko kidogo,